Baada ya uongozi wa Yanga kumaliza changamoto iliyojitokeza baina yake na wachezaji, kikosi cha timu hiyo leo kimeendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Azam Fc
Mchezo huo utapigwa keshokutwa, Jumatatu katika uwanja wa Uhuru
Wachezaji leo wamehudhuria mazoezi kama kawaida isipokuwa Kelvini Yondani na Papi Tshishimbi ambao wana udhuru
Wakati Yondani akiendelea kutumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu, Tshishimbi ni majeruhi
ADVERTISE HERE