Kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa kesho Jumatatu April 29 kwenye uwanja wa Uhuru
Baada ya sintofahamu ya siku mbili, wachezaji wa timu hiyo walirejea rasmi mazoezini jana wakiwa na morali kusaka matokeo katika mchezo huo
Amissi Tambwe, mshambuliaji mwandamizi wa mabingwa hao wa kihistoria amesema mchezo wa kesho una umuhimu wa kipekee kwao kwani wanafahamu kama hawatapata ushindi basi watauweka rehani uongozi wao wa ligi kwani wapinzani wao Simba watahitaji kushinda michezo miwili tu ili wapande kileleni
"Azam Fc ni timu nzuri, najua haitakuwa kazi rahisi kuwafunga lakini sisi tunahitaji kushinda ili tuendelee kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi," amesema
Juzi wakati wachezaji wa kikosi cha kwanza wakifanya mazungumzo na uongozi, Zahera alilazimika kuwaandaa wachezaji wa Yanga B ambapo alikuwa tayari kuwatumia wachezaji hao kesho kama mwafaka usingepatikana kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza