Meneja wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' leo amekabidhiwa fedha taslim Tsh 350,000/- zikiwa ni fedha zilizochangiwa na wadau wa klabu hiyo kama sehemu ya kumshukuru baada ya kuitumikia Yanga kwa muda mrefu akiwa mchezaji
Cannavaro amewashukuru Wanayanga kwa kutambua mchango wake na amewataka kuendeleza utamaduni huo kwa wachezaji wengine wanaofikia mafanikio kama yake
"Nawashukuru sana kwa hiki mlichonipatia, kwangu mimi sio kiasi kidogo. Naomba muendelee hivi hivi sio kwangu mimi tu bali hata kwa wengine wanaofanya vizuri ama kustaafu"
"Kazi yetu ni kuijenga Yanga tuitoe hapa ilipo na tuisogeze mbele zaidi inapotakiwa iwepo," amesema
Mbali na kukabidhiwa kiasi hicho cha fedha, Cannavaro atapokea sehemu nyingine ya fedha iliyotokana na mauzo ya T-Shirt zilizotengenezwa kwa heshima yake baada ya kustaafu