Kampeni za uchaguzi wa klabu ya Yanga zimefunguliwa rasmi leo ambao wagombea wanaanza kunadi sera zao kwa wanachama
Kampeni zitahitimishwa siku moja kabla ya uchaguzi ambao utafanyika Jumapili May 05 2019
Wanachama wa Yanga wameaswa kuwa makini kuhakikisha wanachagua viongozi sahihi ambao wataweza kuiondoa timu hiyo kwenye dimbwi la 'umasikini'
Ili kuweza kuwabaini wagombea wenye sifa, wanachama wameaswa kufuatilia kampeni za wagombea wote, kusikiliza sera zao ili wawe na nafasi ya kufanya uamuzi sahihi siku ya uchaguzi
Wanachama wameaswa wasikubali kununuliwa au kushawishiwa kwa njia yoyote isiyo halali kwani kufanya hivyo sio kuisaidia Yanga
Ushindani mkubwa uko kwenye nafasi za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ambapo wagombea nane wanatarajiwa kuwania nafasi hizo
Wagombea wanaowania nafasi ya Mwenyekiti ni;