Yanga kupata viongozi wapya leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 May 2019
Yanga kupata viongozi wapya leo

Wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika klabu ya Yanga jana walihitimisha zoezi la kampeni kuelekea uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika leo Jumapili ukumbi wa Bwalo la Polisi, Osterbay jijini Dar es salaam

Wagombea walianza kunadi sera zao kwa Wanachama Jumanne iliyopita

Nafasi ya Mwenyekiti wa Yanga inawaniwa na wagombea wawili, Dk Jonas Tiboroha na Dk Mshindo Msolla wakati nafasi ya Makamu Mwenyekiti inawaniwa na wagombea wanne ambao ni Fredrick Mwakalebela, Janeth Mbene, Titus Osoro na Yono Kevela

Aidha wagombea 21 wanawania nafasi nane za wajumbe wa Kamati ya Utendaji

Wanachama wa Yanga wametakiwa kutofanya makosa kwenye uchaguzi wa kesho kwa kuwachagua viongozi ambao wataweza kuipeleka Yanga mbele

Suala la Mabadiliko limekuwa kilio cha Wanayanga. Wagombea wote wameahidi kufanya mabadiliko, ni jukumu la Wanachama kujiridhisha na uwezo wao na ahadi walizotoa katika kutatua changamoto zinazoikabili Yanga

Wanachama wameaswa kutochagua viongozi kwa mazoea badala yake wachague viongozi ambao wana upeo mkubwa

Ni vyema kiongozi atakayechaguliwa awe na uwezo wa kutengeneza mikakati ya kuipeleka Yanga kule ambako kila mdau anahitaji kuona klabu ikielekea

Huu sio wakati wa kujaribu viongozi, Wanachama wawaweke madarakani 'watu wa kazi'

Wanachama wasichague viongozi kwa papara, mihemko na makundi, kila mmoja afanye uamuzi kwa maslahi ya klabu kwa kuchagua viongozi wenye tija

Yanga ikipata viongozi wazuri, utakuwa mwanzo wa kutengeneza Yanga imara ambayo itagombewa na wawekezaji na kuifanya timu hiyo kongwe zaidi Tanzania kuondokana na dimbwi la 'umasikini'

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’