Idadi kubwa ya wanachama wa Yanga tayari wamehakikiwa na kuingia ukumbi wa Bwalo la Polisi, Osterbay wakisubiri kuanza kwa mchakato wa uchaguzi
Kulingana na ratiba iliyotolewa jana, zoezi la kupiga kura litaanza saa sita mchana na litahitimishwa saa tisa Alasiri
Kumekuwa na utulivu mkubwa miongoni mwa Wanachama wengi waliofika kuchagua viongozi
Bila shaka wanachama wanafahamu, uamuzi wao kwenye sanduku la kura utabeba hatma ya Yanga kwa miaka minne ijayo



ADVERTISE HERE