Milioni 20 zachangishwa 'fasta' uchaguzi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 May 2019
Milioni 20 zachangishwa 'fasta' uchaguzi Yanga

Wanachama wa Yanga wameichangia timu yao muda mfupi kabla ya mchakato wa kupiga kura kuanza huku lengo likiwa kukusanya Sh 1.5 Bilioni.

Mwenyekiti wa kamati ya hamasa na michango ya Yanga, Anthony Mavunde alisema mkakati uliokuwepo ni kukusanya Sh1.5 Bilioni na mchakato wa kukusanya utafungwa Mei 18.

Alisema Kamati yao ilikuwa na mpango muda mfupi na kufafanua kwamba Yanga haiombi inachangisha kupitia wanachama.

Kabla ya uchaguzi kuanza, Mavunde alichukua jukumu la kuchangisha kuelekea kwenye mechi ya kesho huku Mavunde akifungua kwa kuchangia Sh 1 Milioni.

Kuchangia kuliendelea kwenye Meza kuu ambapo Lucas Mashuri, Kifukwe, Sam Mapande walichangia Sh1 Milioni kila mmoja.

George Mkuchika alitoa Sh 2 Milioni na Tindwa Beda alitoa Sh 1.5, Ally Mchungahela alitoa Sh 250,000, Seif Gulamali alitoa Dola 200 huku lengo likiwa kukusanya Sh 10 Milioni kwa Meza kuu.

Akizungumzia mchakato wa uchangishaji, Mavunde alisema:

"Tumetengeneza kadi 1500 kila moja ina thamani ya Sh 1 Milioni, tumezigawa kwa makundi na mtu mmoja mmoja.

"Zoezi la limeanza muda mrefu na hamasa ni kubwa, hivyo Mei 18 katika hoteli ya Serena tutakuwa na fundraising kwa ajili ya michango kabla ya zoezi kufungwa na kukabidhi michango kwa uongozi.

Alisema kusudio la Mei 18 ni kukusanya zaidi ya Milioni 500 kabla kufungwa siku hiyo

Kwa hisani ya Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’