Baada ya kupoteza mchezo wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Lipuli jana, kikosi cha Yanga kinaelekea Musoma kuikabili Biashara United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa Ijumaa, May 10 uwanja wa Karume
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla pamoja na viongozi wote waliochaguliwa juzi, walikuwepo dimba la Samora kuipa sapoti timu jana na wameahidi kuwa bega kwa bega na wachezaji pamoja na benchi la ufundi kuhakikisha wanashinda michezo minne iliyobaki
Yanga inaweza kufikisha alama 92 kama itashinda michezo yote minne iliyobaki hata hivyo hatma ya ubingwa itategemea na matokeo ya wapinzani wao Simba ambao wana michezo nane huku wakihitaji alama mbili tu ili kuipiku Yanga kileleni
Yanga imejihakikishia kumaliza nafasi mbili za juu msimu huu baada ya jana Azam Fc kushindwa kupata ushindi dhidi ya Stand United ikilazimishwa sare ya bao 1-1
Azam ina alama 67 na hata ikishinda michezo minne iliyobaki itafikisha alama 79