Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la FA, Yanga imedhamiria kumaliza kwa ushindi wa asilimia 100 michezo minne iliyobaki ligi kuu ya Tanzania Bara
Beki mwandamizi katika kikosi cha Yanga Andrew Vicent amesema kipigo cha Lipuli Fc kimewauma sana lakini wanasahau matokeo hayo na sasa wanaelekeza nguvu zao katika michezo hiyo iliyobaki
Amesema jukumu kubwa walilobaki nalo ni kuhakikisha wanashinda michezo yote bila ya kujali idadi ya michezo ambayo Simba wanayo
"Kupoteza mchezo dhidi ya Lipuli imetuuma sana na mashabiki wetu watuwie radhi kwani tulipambana ila bahati haikuwa kwetu
"Lakini nguvu yetu ya tone la mwisho tutaimalizia kwenye ligi kuu
"Sisi hatutaki kuangalia Simba ina mechi nyingi mkononi, tunacholinda tunaongoza ligi na tunatakiwa kushinda mechi zetu hayo mengine hayatuhusu," Chikupe amenukuliwa na Mwanaspoti
Yanga inaelekea mkoani Mara ambapo Ijumaa itashuka uwanja wa kumbukumbu ya Karume kumenyana na Biashara United