Kikosi cha Yanga tayari kiko mkoani Mwanza safarini kuelekea Musoma kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Biashara United
Mchezo huo utapigwa keshokutwa Ijumaa, May 10 kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume
Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la FA hatua ya nusu fainali kwa kufungwa mabao 2-0 na Lipuli, Yanga imebakisha michezo minne ya ligi kumaliza msimu
Ikimaliza mchezo dhidi ya Biashara United, michezo mingine mitatu itakayobaki yote itapigwa jijini Dar es salaam
Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Mwinyi Zahera amesema wanahitaji kumaliza msimu kwa kushinda michezo yote minne
ADVERTISE HERE