Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema TFF iliiandalia Simba ubingwa ndio maana wamepanga kuwakabidhi kombe kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Sevilla May 23
Kwa mujibu wa kauli aliyoitoa msemaji wa Simba Haji Manara hivi karibuni, kuwa wataomba wakabidhiwe taji la ligi kuu siku watakayocheza na Sevilla
"Hili la Manara kusema kwamba wapatiwe kombe wakati Sevilla amekuja manaa yake ni kwamba anafahamu mpango uliopo. Mimi siwezi kusema Simba amebeba kombe, ila Simba amepewa kombe" amesema Zahera
Baada ya kumaliza ratiba ya mkoani Mbeya, Simba ilipangiwa kucheza michezo mitano mfululizo jijini Dar es salaam. Kama ingeshinda michezo yote, basi ingeweza kutwaa ubingwa kabla ya kucheza na Sevilla
Hata hivyo kama Yanga itapoteza mchezo dhidi ya Ruvu Shooting leo, na Simba ikashinda michezo miwili dhidi ya Mtibwa Sugar na Ndanda, basi itaweza kutwaa ubingwa kabla ya May 23 na huenda wakakabidhiwa taji watakapocheza na Sevilla