Makambo atimkia Guinea, ajiunga na Horoya Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 May 2019
Makambo atimkia Guinea, ajiunga na Horoya Fc

Mshambuliaji wa Yanga Heritier Makambo ametimkia Guinea kujiunga na klabu ya Horoya Fc

Taarifa za Makambo kusajiliwa na Horoya zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii mapema leo ambapo timu hiyo imemtambulisha rasmi

Makambo ndiye kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga msimu huu akitupia kambani mabao 16

Kulingana na mtandao wa Kalonews, Makambo amesaini mkataba wa miaka mitatu

"Horoya AC imemsajili mshambuliaji kutoka DR Congo Heritier Makambo aliyekuwa akiichezea Young Africans ya Tanzania," imesema taarifa ya mtandao huo

"Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aliyewahi kuichezea Motema Pembe, amefunga mabao 16 kwenye ligi ya Tanzania"

"Amesaini mkataba wa miaka mitatu"

Kuondoka kwa mshambuliaji huyo ni pigo kwa Yanga ambayo iko kwenye mchakato wa kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao

cut

Yanga italazimika kuingia sokoni kusaka washambuliaji wengine wakali

Hata hivyo Yanga itanufaika na mauzo ya mshambuliaji huyo kwani mkataba wake na Yanga ulikuwa bado haujamalizika

Inaelezwa Makambo ameuzwa kwa dau linalokadiriwa kufikia Milioni 230 za Kitanzania

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’