Winga wa zamani wa Yanga Emmanuel Martin amemsifia beki mkongwe Kelvin Yondani kuwa beki huyo anazidi kuwa bora kadiri umri unavyosonga mbele
Martin aliyeachwa na Yanga wakati wa usajili wa dirisha dogo na kutua Ruvu Shooting, amesema tangu alipofahamu Yondani, uwezo wake haukupungua
Martin amefichua kuwa walishindwa kupata ushindi mchezo dhidi ya Yanga mapema wiki hii kutokana na Yondani kuwaharibia mipango mara kwa mara
"Unajua Yanga wanaweza wakamuona Yondani kama mchezaji wa kawaida, ila kwetu washambuliaji tunajua jinsi anavyotutibulia mipango ya kufunga, Yanga isipomuandaa mapema mbadala wake wakiachana naye watapata tabu sana. Watayumba," amesema
Yondani ni mmoja wa wachezaji waandamizi wa kikosi cha Yanga waliodumu klabuni hapo kwa muda mrefu
cutLicha ya changamoto za kiuchumi zinazoikabili Yanga, Yondani ameendelea kubaki Jangwani
Kutokana na uwezo wake angeweza kujiunga na timu nyingine lakini hata hivyo anafurahia maisha katika klabu ya Yanga
Mwaka jana alisaini mkataba wa miaka miwili ambao utamuweka Jangwani hadi mwakani
Ni miongoni mwa wachezaji wa kutegemewa wa kikosi cha timu ya Taifa "Taifa Stars" ambacho mwezi ujao kitaelekea Misri kushiriki fainali za michuano ya AFCON 2019