Uongozi wa Yanga jana ulitumia hafla ya Iftar Gala Dinner iliyofanyika Serena Hotel kuwapongeza wachezaji pia kuwakutanisha wadau wa Yanga kujadiliana masuala mbalimbali yanayoihusu klabu hiyo
Kamati ya hamasa inayoongozwa na Mh Anthony Mavunde imetangaza tukio kubwa la kuhitimisha kampeni ya uchangiaji Yanga litafanyika Juni 15 mwaka huu ukumbi wa Diamond Jubelee jijini Dar es salaam
Tukio hilo liliondolewa kwenye hafla ya jana kutokana na kuendelea kwa mfungo wa mezi mtukufu wa Ramadhani
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alisema isingekuwa vizuri kuendesha tukio hilo wakati huu ambao sehemu kubwa ya wadau wake wako katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani
ADVERTISE HERE