Waziri wa nchi TAMISEMI Mh Suleiman Jaffo amesema timu ya Yanga ilistahili kuwa mabingwa msimu huu kutokana na kushiriki ligi katika mazingira magumu lakini bado ikafanya vizuri
Mh Jaffo ameifananisha Yanga na mtoto aliyekosa ada shuleni lakini akawa na maendelea mazuri na kufaulu mitihani
"Tumeona timu ambayo inapata ufadhili mkubwa sana Simba, lakini mwaka huu huu tumeona timu ambayo hata maisha yake ni ya shida, ya kubahatisha lakini kila siku ilikuwa inapiga watu, timu ya Yanga"
"Yanga mwaka huu ni sawasawa na mtoto aliyekosa ada shuleni lakini darasani anaongoza"
"Ukiangalia, ukafanya tathmini ya kimichezo, bingwa mwaka huu ni Yanga"
"Kama unafanya tathmini ya kweli ya kimichezo, yani Yanga mwaka huu kama ni mtoto aliyekosa ada, akifika darasani anasoma akiwa na msongo wa mawazo hajui inawezekana mda wowote atafukuzwa shuleni. Hana amani hata kidogo lakini mtihami ukija ana A""Halafu huku kuna mwingine anakula mkate wa 'blubendi' na nini halafu hata ratiba zote anafanyiwa yeye"
ADVERTISE HERE