Kiungo Papi Tshishimbi jana alisaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kubaki Yanga hivyo kuondoa tetesi kuhusu hatma yake
Inaelezwa Tshishimbi alikuwa na ofa tatu mezani, moja ikiwa timu ya hapa nyumbani na mbili zikiwa kutoka ligi kuu ya Afrika Kusini
Kutokana na umuhimu wa kiungo huyo, mabosi wa Yanga kwa haraka jana walimalizana nae akisaini mkataba wa miaka miwili mbele ya Makamu Mwenyekiti Fredrick Mwakalebela, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Frank Kamugisha na Mwanasheria wa Yanga Abdallah Lyana
Mabadiliko yamshawishi kubaki Yanga
Baada ya kusaini mkataba mpya, Tshishimbi amesema ameona mambo mazuri yanakuja Yanga hivyo anataka kuwa sehemu ya kikosi kitakachorejesha heshima ya timu hiyo msimu ujao
"Mambo yameanza kubadilika Yanga ndio maana nimeamua kuendelea kubakia hapa," amsema
"Natambua tuna kazi kubwa ya kuirejesha heshima ya timu yetu msimu ujao"