FT : Yanga 0-2 Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 May 2019
FT : Yanga 0-2 Azam Fc

Yanga imemaliza vibaya ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2018/19 baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Azam Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa

Mabao ya Daniel Amoah na Mudathir Yahya yalitosha kuihakikishia Azam Fc ushindi ikilipa kisasi cha kipigo cha bao 1-0 cha mchezo wa duru ya kwanza

Yanga ilikuwa bora kwenye kipindi cha kwanza lakini ilishindwa kuzitumia nafasi chache ilizotengeneza

Matokeo hayo hayabadili chochote kwenye msimamo wa ligi ambapo Yanga imemaliza katika nafasi ya pili ikiwa na alama 86 wakati Azam Fc imefikisha alama 75 na kubakia katika nafasi ya tatu

Ulikuwa ni msimu uliojaa changamoto nyingi kwa kikosi cha Yanga lakini hatimaye umemalizika salama

Mshambuliaji Heritier Makambo ameaga rasmi kunako klabu hiyo akimaliza msimu kwa kuifunga mabao 17

Makambo anakwenda kujiunga na klabu ya Horoya AC

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amesema morali ya wachezaji wake ilikuwa chini leo pengine ni kutokana na mchezo huo kutokuwa na umuhimu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
1h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
13h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
22h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’