Yanga leo imetumia uwanja wa Majimaji kufanya mazoezi kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya wenyeji, Majimaji kesho Septemba 16.
Kikosi cha Yanga kiliwasili mapema jana kikitokea Njombe, wachezaji walipewa mapumziko baada ya kukosekana uwanja mzuri wa kufanyia mazoezi.
Changamoto hiyo ilimlazimu Lwandamina asitishe mazoezi baada ya kukataliwa kutumia uwanja wa Majimaji utakaotumika kwenye mchezo huo.
Mchezo wa mzunguuko wa tatu ligi ya Vodacom kati ya wenyeji Majimaji dhidi ya Yanga utapigwa kwenye dimba la Majimaji kuanzia saa kumi jioni.
Hautakuwa mchezo mwepesi kwa Yanga, lakini kocha Lwandamina anaamini kikosi chake kinatarajiwa kuondoa na alama zote tatu.
Msimu uliopita Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika uwanja huo, Deus Kaseke akifunga bao hilo pekee.

ADVERTISE HERE