Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaya amesema timu hiyo imemuuza mshambuliaji wake Heritier Makambo kwenda klabu ya Horoya AC kwa dau la euro 70,000 ambazo ni zaidi ya Tsh Milioni 180
Makambo aliondoka nchini baada ya ligi kumalizika kuanza maisha mapya nchini Guinea
Aidha, licha ya kupokea ofa nono zaidi kutoka Ubelgiji kwa ajili ya mshambuliaji huyo huyo aliyetua Yanga kwa dau la Milioni 45, Kaya amesema waliamua kumuuza Horoya kwa kuwa ofa hiyo ilichelewa
"Horoya walileta ofa ya Euro 70,000 na kwa kulinganisha na bei tuliyomnunulia ya Euro 17,000 tuliona ni biashara nzuri," alisema Kaya
"Lakini pia tuliona timu ina uhitaji wa pesa, tuna mchakato wa usajili wa wachezaji wapya na wachezaji wengine wamemaliza mikataba tunahitaji kuwasainisha mikataba mipya"
"Tulipokea ofa nyingine kutoka Ubelgiji ambayo ilikuwa nono zaidi lakini kwa bahati mbaya ilifika wakati mchakato wa Horoya ukiwa uko karibu kumalizika"
cutMakambo ameitumikia Yanga kwa msimu mmoja lakini ameacha alama akifunga mabao 23 katika michezo 42
Alimaliza nafasi ya tatu katika mbio za ufungaji bora ligi kuu akifunga mabao 17 nyuma ya Salim Aiyee (18) na Meddie Kagere (23)
Baada ya kumuuza Makambo Yanga imedhamiria kuboresha safu yake ya ushambuliaji ambapo tayari imekamilisha usajili wa Maybin Kalengo aliyetokea ZESCO United
Pia iko mbioni kukamilisha usajili wa mshambuliaji mzawa Mapinduzi Balama ambaye msimu uliomalizika aliitumikia Alliance FC