Namungo Fc yamuwania Kabwili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jun 2019
Namungo Fc yamuwania Kabwili

Mlinda lango wa Yanga Ramadhani Kabwili anatajwa kuwaniwa na Namungo Fc ya mkoani Lindi ambayo itashiriki ligi kuu msimu ujao ikiwa imepanda daraja msimu huu

Kabwili aliyepata nafasi ya kubwa ya kucheza kwenye kikosi cha Yanga msimu huu baada ya timu hiyo kuachana na Beno Kakolanya, amemaliza mkataba lakini inaelezwa bado Yanga inaweza kumbakisha kwa kumpa mkataba mpya

Yanga iko kwenye mchakato wa kuboresha eneo la golikipa ambapo tayari imemsajili kipa wa Bandari Fc Farouq Shikalo

Aidha inaelezwa Yanga pia imekamilisha usajili wa mlinda lango wa Azam Fc aliyekuwa akicheza kwa mkopo klabu ya Mbao Fc Metacha Mnata

Tangu juzi viongozi wa Yanga walikuwa wakihaha kumsajili kipa huyo kabla hajajiunga na kambi ya timu ya Taifa

Baada ya usajili wa makipa hao, nafasi ya Kabwili imezidi kuwa finyu na huenda akaondoka

Namungo pia inaweza kumchukua kwa mkopo kinda Gustapha Saimon aliyepandishwa kikosi cha kwanza na kocha Mwinyi Zahera

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’