Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinatarajiwa kuondoka wakati wowote kuelekea nchini Misri ambako kitaendelea na kambi ya kujiandaa na fainal za AFCON 2019 zitakazofanyika baadae mwezi huu nchini humo
Kocha Mkuu wa Stars Emmanuel Amunike amependekeza kambi ya Stars kuweka nchini Misri ambako ndiko michuano ya AFCON itafanyika
Taarifa za awali zimebainisha kuwa Amunike anatarajiwa kuondoka na nyota 32 kuelekea nchini Misri
Kwa sasa Stars imeweka kambi Whitesands hotel jijini Dar es salaam ikijifua katika uwanja wa Taifa ikiwa na nyota wote 39 walioteuliwa kuunda kikosi cha awali
Nyota saba wanatarajiwa kuachwa kwenye safari hiyo
Mkurugenzi wa michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusuph Singo amethibitisha taarifa ya Stars kuelekea nchini Misri
"Serikali ipo karibu kabisa na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania katika maandalizi yote, tunafanya mpango wa pamoja kuhakikisha timu yetu inapata kambi nje ya hapa wakiwa wanajiandaa kwa masbindano ya AFCON na itakuwa kulele Misri," amesema
"Kama hakutakuwa na mabadiliko timu itaondoka hivi karibuni, hayo ni mapendekezo ya kocha, tulifikiria kuipeleka nchi nyingine lakini mwalimu akasema tuweke kambi kule ambako yatafanyika mashindano"