Mzuka wa Wanayanga umepanda baada ya timu yao kupata nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao
Yanga iliyomaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, haikuwa na matumaini ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao baada ya kukosa ubingwa na kushindwa kutwaa kombe la FA
Hata hivyo timu hiyo inayonolewa na kocha Mwinyi Zahera, licha ya changamoto ilizopitia, ilijiwekea lengo la kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa iwe kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ama kombe la FA
Feisal Salum 'Fei Toto', kiungo fundi wa Yanga amesema klabu hiyo kupata nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa mwaka huu ni faraja kwa mashabiki wao ambao walikuwa na hamu kuona jambo hilo.
cut"Kila mdau aliona namna ambavyo Yanga tulikuwa tumepambana kwa nguvu zetu zote kuchukua ubingwa, ilishindikana tukaishia nafasi ya pili.
"Hamu yetu ilikuwa ni kushiriki michuano ya kimataifa, lakini kwa kuwa limetokea hili ni jambo la heri kwa klabu yetu pia faraja sana kwa mashabiki kuona timu yao ina majukumu ya kimataifa"
Yanga inapaswa kuanza maandalizi mapema kufuatia mabadiliko ya kalenda ya michuano ya CAF ambapo mechi zinatarajiwa kuanza mwezi Agosti 2019
Michezo ya hatua ya awali itapigwa kati ya Agosti 9-11 na michezo ya marudiano kupigwa mwishoni mwa mwezi wa nane