Mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Majimaji dhidi ya Yanga uliopigwa kwenye dimba la Majimaji umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
Majimaji wakicheza nyumbani walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kwenye dakika ya 53 mfungaji akiwa Peter Mapunda akipiga shuti nje kidogo ya 18.
Yanga ilisawazisha kwenye dakika ya 79, mfungaji akiwa Donald Ngoma aliyeunganisha vyema krosi ya Obrey Chirwa.
Hali ya uwanja ilikuwa kikwazo kikubwa kwa mabingwa wa soka Tanzania Bara kuonyesha kiwango kwani haikuwa rahisi kwa dimba hilo kupiga pasi za chinichini.
Wenyeji Majimaji walitoa upinzani wa hali ya juu kwa mabingwa na hakika msimu huu unaweza kusema hakuna timu kibonde.
Baada ya mchezo huo kocha msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema ingawa timu yake ilipania kuondoka na alama zote tatu, wameridhika matokeo hayo waliyopata ugenini.
Aidha katika mchezo huo winga Emanuel Martini alipata majeraha yaliyomlazimu akimbizwe Hospitalini.
Matokeo ya michezo mingine
Mtibwa 2-1 Mbao
Prisons 0-0 Ndanda
Lipuli 0-0 Ruvu Shooting
Stand 0 -1 Singida

ADVERTISE HERE