Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya waamuzi watakaochezesha michuano ya Kombe la Afrika nchini Misri lakini hakuna hata mwamuzi mmoja kutoka Tanzania aliyebahatika kuwemo kwenye orodha hiyo.
Katika orodha iliyotolewa na CAF wiki iliyopita, jumla ya waamuzi 56 kutoka nchi mbalimbali Afrika wameteuliwa ambapo 26 ni wa kati na wengine ni waamuzi wasaidizi.
Timu ya Burundi inayoshiriki AFCON kwa mara ya kwanza imebahatika kumtoa mwamuzi wa kati wa kimataifa, Ndabihawenimana Pacifique, huku Kenya ikijivunia Peter Waweru na Rwanda licha ya timu yao ya taifa kushindwa kufuzu, wamefanikiwa kumtoa refa wa kati, Louis Hakizimana.
Kenya pia inayo mwamuzi msaidizi Gilbert Cheruiyot kwenye orodha hiyo ya CAF mwamuzi mwingine msaidizi kutoka Afrika Mashariki akiwa Mark Ssonko kutoka Uganda.
Misri na Tunisia ndiyo wanaoongoza kuwa na idadi kubwa ya waamuzi kwenye AFCON ya mwaka huu, watano kila nchi wakifuatiwa na Morocco ambao wana waamuzi wanne huku CAF ikishindwa kumteua hata mwamuzi moja kutoka Nigeria