Jumamosi ijao Juni 15 2019 Yanga inatarajiwa kufanya tukio la kihistoria ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam kwa kuendesha Harambee kubwa iliyopachikwa jina la KUBWA KULIKO
Harambee hiyo imeitwa KUBWA KULIKO kwa sababu itawakutanisha wadau wote wa Yanga bila ya kujali rika, cheo, umaarufu, umasikini wala utajiri wao kwenye hafla muhimu ya kuiwezesha timu yao
Tiketi zimeendelea kuuzwa kupitia mitandao ya simu, Tigopesa na Mpesa ambapo kuanzia leo Jumanne zitaanza kuuzwa katika vituo mbalimbali kama ilivyoainisha kwenye taarifa iliyotolea na uongozi wa Yanga jana
Hiyo ni siku maalum kwa Wanayanga kumaliza machungu ya timu yao ya misimu miwili iliyopita kwa kuifanya izaliwe upya ikiwa imara mara dufu
Mpaka sasa Wanayanga wamefanya kazi kubwa ya kufanikisha usajili wa baadhi ya wachezaji, lakini baada ya Harambee hiyo inaelezwa sajili kubwa za kutikisha nchi zitafanywa
Siku hiyo baadhi ya wachezaji ambao tayari wamemwaga wino kunako klabu hiyo watawekwa hadharani
Pia inaelezwa Juni 15 inaweza ikawa siku ya furaha zaidi kwa Wanayanga kwani mchezaji mmoja ambaye usajili wake utatikisa nchi huenda akatangazwa
Yanga imekuwa ikihusishwa na nyota kadhaa kutoka nje ya nchini na wengine kutoka hata kwa watani zao Simba, siku hiyo huenda 'jipu likapasuliwa'