Ali Yanga azikwa Shinyanga

Admin By Admin
β€’
22 Jun 2017
Ali Yanga azikwa Shinyanga
TAARIFA KWA UMMA

Uongozi wa klabu ya Yanga kwa heshima na taadhima unapenda kuwataarifu wadau wa soka nchini kuwa leo asubuhi mpendwa wetu Ally Yanga alipumzishwa katika nyumba yake ya milele mkoani kwao Shinyanga.

Klabu iliwakilishwa na mjumbe wa kamati ya Utendaji Samwel Lukumai, wanamichezo na wana Yanga wote wa Shinyanga na mikoa ya karibu.

Pia uongozi unatumia fursa hii kumshukuru mpendwa Raisi wetu wa jamhuri ya Muungano Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwa kuguswa kwake na msiba huu wa mwanamichezo na mwana Yanga mwenzetu na kututumia salamu za rambirambi.

Kwa niaba ya wanachama Uongozi umepokea salamu hizo kwa unyenyekevu mkubwa na kuingiwa na faraja kuona kiongozi mkuu wa nchi yupo pamoja nasi katika msiba huu.

Hii inaonesha jinsi gani raisi anavyojali na kuguswa na wanamichezo.

Daima klabu ya Yanga itakumbuka mchango wa Ally Yanga kama mwanachama mwandamizi ambaye aliyatoa maisha yake kuitumikia klabu yetu katika upande wa ushangiliaji.

Klabu inasisitiza tuendelee kuiombea faraja familia yake katika kipindi hiki chote cha Majonzi.

Asanteni.

Imetolewa na idara ya habari na mawasiliano
Young African Sports Club.
22.06.2017
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’