Wakati mzunguuko wa tatu wa ligi kuu ya Vodacom ukitarajiwa kukamilika leo kwa Simba kuchuana na Mwadui kwenye dimba la Uhuru na Mbeya City kuwa mwenyeji wa Njombe Mji, ni Mtibwa Sugar pekee iliyoshinda michezo yake yote mitatu ya mwanzo.

Ligi ya msimu huu inaonekana kuwa na ushindani mkali, Ingawa bado ni mapema kutabiri nini kitatokea, lakini kuna kila dalili kuwa baadhi ya timu ambazo hazipewi nafasi zitafanya vizuri.
Moja ya timu hizo ni Mtibwa Sugar ambayo tayari iko kileleni mwa msimamo ikiwa na rekodi ya kushinda kwa asilimia 100.
Msimu huu vita ya ubingwa wa VPL haitakuwa ya timu mbili au tatu kama ilivyozoeleka. Timu zote zikiwemo zilizopanda daraja zinaonyesha viwango vizuri.
Hata hiyo Ruvu Shooting iliyofungwa mabao 7-0 kwenye mchezo wa kwanza sio mbovu, kilichowatokea ni 'ajali' kwenye soka kama msemaji wao alivyoita kipigo hicho.
Haijapoteza mchezo mwingine tena, imepata sare za ugenini kwenye mcihezo yake miwili.

ADVERTISE HERE