Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Harambee ya kuichangia Yanga maarufu kama Kubwa Kuliko itakayofanyika kesho Jumamosi ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
Tukio hilo lililobeba sura ya kitaifa litawakutanisha wadau wa Yanga na wasio wadau ambao wamealikwa kushiriki
Miongoni mwa wageni Maalum watakaohudhuria ni Rais Mstaafu wa Awamu nne Dk Jakaya Kikwete ambaye amethibitisha kuwa atashiriki
Kwa wale waliokuwa wakibeza kampeni ya kuichangia Yanga huenda kesho wasiamini kile kitakachotokea ukumbi wa Diamond Jubilee
Kamati ya Hamasa na Uchangishaji kesho itahitimisha kazi yake kwa kuweka hadharani kiasi cha fedha ambazo zimekusanya tangu kuundwa kwa Kamati hiyo miezi miwili iliyopita na kisha kuukabidhi uongozi wa Yanga
Aidha, lengo la makusanyo ya fedha katika Harambee ya Kubwa Kuliko hapo kesho ni Tsh Bilioni 1.5 au zaidi
Yanga imedhamiria kukiimarisha kikosi chake kazi ambayo tayari imeanza kufanyika
Baada ya Harambee ya kesho, Yanga itakamilisha michakato ya usajili iliyokuwa imebaki