Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa ameichangia Yanga Tsh Milioni 10 fedha ambazo alizotoa hapohapo ukumbi wa Diamond Jubilee katika hafla ya kuichangia Yanga maarufu kama KUBWA KULIKO
Mh Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo, pia amesema alizungumza na mfanyabiashara Rostam Aziz ambaye kwa sasa yuko nchini Marekani
Rostam ameahidi kuichangia Yanga Tsh Milioni 200
Aidha Rostam akirejea nchini ametaka kuonana na viongozi wa Yanga ili kuweka mkakati wa kuisaidia zaidi timu hiyo
Katika hotuba yake aliyoitoa kwa Wana Yanga, Mh Majaliwa amesisitiza umoja na ushirikiano huku akiutaka uongozi wa Yanga kuweka mipango thabiti itakayoweza kuifanya Yanga iondokane kabisa na changamoto kama zilizoikumba msimu uliopita