Sonso aomba kusaini baada ya AFCON

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jun 2019
Sonso aomba kusaini baada ya AFCON

Beki anayemaliza mkataba kunako klabu ya Lipuli Fc Ally Mtoni 'Sonso' ameomba kusaini mkataba kuitumikia Yanga baada ya kumalizika kwa michuano ya AFCON 2019, imefahamika

Mtoni alishamalizana na uongozi wa Yanga kilichokuwa kimebaki ni yeye kusaini mkataba zoezi ambalo ameomba lifanyike baada ya AFCON

Beki huyo kisiki aliyepenya kwenye kikosi cha wachezaji 23 watakaoiwakilisha Tanzania huko Misri, amesema amekuwa na ndoto ya kucheza soka nje ya nchi pengine michuano ya AFCON inaweza kumfanya akatimiza ndoto hiyo

"Niliwaomba viongozi wa Yanga kwa vile tumeshakubaliana kila kitu, wanisubiri nimalize kwanza jukumu ya Misri, kisha mengine yatafuata. Sikutaka kukurupuka kwa vile haya ni maisha ukijichanganya tu wakati mwingine inakula kwako" Sonso amenukuliwa na Mwanaspoti

"Mashindano haya ya Afcon kama mchezaji unapata nafasi ya kucheza na ukafanya vizuri unaweza kuwashawishi viongozi na makocha wa timu nyingine kupata wazo la kukusajili, hivyo nimeona ni vyema kucheza Afcon nikiwa huru na baada ya kumalizika ndio hatma yangu itafahamika"

Mpaka sasa Yanga tayari imekamilisha usajili wa mabeki wawili wa kigeni Lamine Moro na Mustapha Suleyman

Kocha Mwinyi Zahera amepania kuimarisha safu yake ya ulinzi ambayo msimu uliomalizika iliwategemea Kelvin Yondani, Andrew Vicent na Abdallah Shaibu 'Ninja'

Kuna taarifa Yanga imepanga kumuongezea mkataba Ninja kisha kumtoa kwa mkopo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’