Kiungo Thabani Kamusoko muasisi wa 'kampa-kampatena' yuko nchini Misri na kikosi cha Zimbabwe ambacho kitashiriki fainali za AFCON 2019 kama ilivyo kwa Tanzania
Jana Tanzania na Zimbabwe zilicheza mchezo wa kirafiki uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1
Baada ya mchezo huo Kamusoko alipata nafasi ya kukutana na baadhi ya nyota aliocheza nao Yanga
"Mchezo ulikuwa mzuri kila timu ilionyesha ushindani. Kwangu mimi nimefurahi zaidi kwa kuwa nimekutana na ndugu zangu," alisema Kamusoko ambaye ameweza kuifahamu lugha ya kiswahili kwa ufasaha kabisa
Ni bahati mbaya tu Kamusoko hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao baada ya mkataba wake kumalizika, lakini ni mchezaji ambaye ataendelea kubaki mioyoni mwa mashabiki wa Yanga
Kuna taarifa klabu ya Gor Mahia imejitosa kumuwania mkongwe huyo ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika