Msimu uliopita Yanga ilikuwa na washambuliaji wa kati wawili tu, Heritier Makambo na Amissi Tambwe
Kikosi cha Mwinyi Zahera kilikuwa na changamoto kubwa kwenye safu ya ushambuliaji.
Mafanikio yaliyopatikana kwa kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi msimu uliopita yalitokana na juhudi kubwa iliyofanywa na wachezaji pamoja na benchi la ufundi
Usajili uliofanywa mpaka sasa tayari umeonekana kutatua tatizo hilo
Juma Balinya, Maybin Kalengo na Sadney Urikhob hawa ni washambuliaji wa kati
Lakini pia Issa Bigirimana na Patrick Sibomana nao wanaweza kucheza nafasi hiyo licha ya kuwa viungo wa ushambuliaji ambao wanatokea pembeni
Inavyoonekana, msimu ujao Yanga itakuwa na kikosi kipana, kila nafasi itakuwa na angalau wachezaji wawili ambao wanaimudu vyema
Hivi ndivyo inayotakiwa Yanga iwe msimu ujao kwani itakabiliwa na mashindano matatu ligi, ligi ya mabingwa na kombe la FA
Aidha changamoto ya ratiba iliyojitokeza msimu uliomalizika, itafanya Bodi ya ligi iwe makini msimu ujao ambapo suala la michezo ya viporo litapunguzwa kwa kiasi kikubwa
Timu zitakazoshiriki michuano ya Kimataifa wakati mwingine zitakabiliwa na changamoto ya kucheza michezo yao karibu karibu
Hapa ndipo umuhimu wa kuwa na kikosi kipana utaonekana