Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa Julai 07 2019
Aidha maandalizi hayo pia yatakuwa maalum kwa ajili ya mchezo wa Kimataifa wa kirafiki siku ya Mwananchi utakaopigwa uwanja wa Taifa, Julai 27
Yanga itaanza mazoezi chini ya kocha Msaidizi Noel Mwandila kutokana na kocha Mkuu Mwinyi Zahera kuendelea na majukumu ya timu ya Taifa ya DR Congo inayoshiriki fainali za AFCON 2019
Aidha baadhi ya nyota wanaoshiriki michuano hiyo huenda wakachelewa kuanza mazoezi kutegemea na hatua ambayo timu zao za Taifa zitafikia huko Misri
Michuano ya Afcon itafika tamati Julai 21 kwa mchezo wa fainali kupigwa
Yanga inatarajiwa kuweka kambi nje ya nchi ambapo uongozi wa timu hiyo umesema mapendekezo ya wapi timu itaweke kambi yatatolewa na Zahera