Wiki ijayo Yanga itaweka hadharani majina ya wachezaji ambao hawataendelea kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amewahakikishia wachezaji wote wenye madai kuwa watalipwa stahiki zao ili waondoke Yanga bila ya kuwa na kinyongo
"Kila mchezaji ambaye ana madai atalipwa. Tunathamini mchango wao na hauwezi kujua siku zijazo yawezekana klabu ikamhitaji tena, akiondoka vizuri ataendelea kuwa na mapenzi na timu yetu," amesema
Aidha uongozi wa Yanga umepanga kuwafanyia tafrija maalum ya kuwaaga wachezaji hao ambao waliitumikia Yanga kwa mapenzi makubwa licha ya changamoto zilizokuwa zikiikabili klabu
Wiki iliyopita Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela alisema wanatambua na kuthamini mchango wa wachezaji wote walioutoa msimu uliopita licha ya kukabiliwa na mazingira magumu sana
Hivyo hawatawaacha hivi hivi