Beki Kelvin Yondani ameeleza furaha yake baada ya Yanga kufanya usajili wa walinzi wapya wa kati
Mabeki Lamine Moro, Mustapha Suleyman, Ally Ally tayari wamekamilisha usajili wao Yanga huku Ally Mtoni akiatarajiwa kumalizana na mabingwa hao wa kihistoria baada ya Afcon
"Ninafurahia maboresho yanayoendelea kufanywa na uongozi katika usajili wao, niwapongeze kwa maboresho makubwa ya kwenye safu ya ulinzi, kiukweli kulikuwa na upungufu mkubwa katika msimu uliopita," Yondani amenukuliwa na Championi
"Lakini nashukuru viongozi wameona upungufu huo kwa kusajili mabeki hao wengine wapya watatu na uzuri kuwa wote tunafahamiana labda huyo mwingine kutoka Burundi lakini Ally na Sonso wote tupo Taifa Stars, licha ya Ally kupunguzwa dakika za mwisho
"Hivyo, msimu ujao utakuwa mzuri kwetu, tutapigania kutwaa ubingwa wa ligi kuu pamoja na kufanya vizuri michuano ya kimataifa,” alisema Yondani aliyekuwa kwenye kikosi cha stars ambacho leo kitacheza na Senegal huko Misri
Pamoja na usajili huo wa mabeki wapya, msimu ujao kikosi cha Yanga kitaendelea kuwa na Yondani na Andrew Vicent ambao bado wana mikataba wakati Abdallah Shaibu anasubiri kujua hatma yake baada ya mkataba wake kumalizika