Yanga ina siku nne za kukamilisha usajili wa CAF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Jun 2019
Yanga ina siku nne za kukamilisha usajili wa CAF

Wakati viongozi wa Yanga wakiwa 'busy' kukamilisha usajili wa timu hiyo kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa, siku nne zimebaki kwa zoezi hilo kufikia tamati

Juni 30 ndio siku ya mwisho kwa timu zinazoshiriki michuano ya CAF msimu ujao kuwasilisha vikosi vyao

Idadi ya wachezaji wanaoruhusiwa kuandikishwa ni 30, hata hivyo timu zinashauriwa kutosajili nafasi zote ili kuweza kuongeza wachezaji hatua ya makundi

Hatua ya awali timu inaweza kusajili kuanzia wachezaji 23 na kuendelea ambapo kwa timu ambayo haitajaza nafasi zote 30 inaweza kutumia nafasi zilizobaki kuongeza wachezaji kwenye hatua ya makundi

Kuanzia mwaka huu kalenda ya michuano ya CAF imebadilika ambapo itaanza mwezi wa nane na kufikia tamati mwezi wa tano mwakani

Michezo ya hatua ya awali itapigwa kati ya Agosti 9-11 na michezo ya marudiano kupigwa Agosti 23-25

Michezo ya raundi ya kwanza itapigwa kati ya 13-15 Septemba na michezo ya marudiano kupigwa 27-29 Septemba

Michezo ya hatua ya makundi itaanza kupigwa mwishoni mwa mwezi wa 11

Kutokana na mabadiliko hayo, kikosi cha Yanga kinapaswa kuingia kambini mapema ambapo uongozi wa timu hiyo tayari umetangaza kambi itaanza Julai 07

Hata hivyo Yanga huenda ikaanza kambi bila ya kocha wake Mkuu Mwinyi Zahera anayekabiliwa na majukumu ya timu ya Taifa huko Misri

Zahera atakosekana zaidi kama DR Congo itafuzu hatua ya mtoano.

Lakini anaweza kuiwahi kambi hiyo kama DR Congo haitavuka hatua ya makundi

Yanga pia itawakosa baadhi ya wachezaji wanaoshiriki michuano hiyo, hatma yao itategemea na hatua ambayo timu zao zitafika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’