Mshambuliaji wa Ndanda Fc Vitalis Mayanga amesema licha ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Yanga, bado hajasaini mkataba na anasubiri simu ya mabosi wa timu hiyo
Mayanga aliyemaliza mkataba Ndanda Fc, amesema bado hajasaini timu yoyote na atakuwa tayari kufanya hivyo baada ya ukimya kutawala katika dili la kutua Yanga
Mshambuliaji huyo aliyeifungia Ndanda Fc mabao 10 msimu uliomalizika, ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakifuatiliwa kwa karibu na Yanga
Hata hivyo huenda uongozi wa Yanga umeachana nae baada ya kukamilisha usajili wa washambuliaji watatu wa kigeni
Washambuliaji waliosajiliwa na Yanga ni Maybin Kalengo (Zambia), Sadney Urikhob (Namibia) na Juma Balinya (Uganda)
ADVERTISE HERE