Yanga ilipata mafanikio makubwa ikiwa chini ya kocha Hans van Pluijm kwa kutwaa mataji mawili ya VPL huku pia kwenye msimu wake wa pili akitwaa mataji yote Yanga iliyoshiriki.
Aidha katika msimu huo Yanga ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi kombe la shirikisho barani Afrika.
Michuano ya kombe la shirikisho kilikuwa chanzo cha Yanga kufanya mabadiliko ya benchi lake la Ufundi.
Wakati huo Yanga ikiwa bado chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wake, Yusuph Manji, malengo ambayo yaliwekwa uongozi wake ilikuwa kuhakikisha Yanga inafanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa.
Wakati wa Pluijm Yanga ilikuwa ikifanya vizuri sana kwenye michuano ya ndani lakini ile michuano ya kombe la shirikisho ilianika udhaifu wa Yanga kwenye medani ya Kimataifa.
Katika michuano ile, Yanga ilimaliza mkiani kundi B ikiwa imejikusanyia alama nne pekee.
Nadhani mashabiki wanaweza wakarudisha kumbukumbu zao nyuma wakati ule ambao Yanga ilikuwa inaburuzwa na vigogo wa soka barani Afrika na ndio kipindi ambacho yalianza mashinikizo ya kutafutwa kocha mwingine kwa kuwa uwezo wa Pluijm ulikuwa umefika kikomo
Ni Yusuph Manji aliyefanikisha kuwasili kwa George Lwandamina ambaye msimu huo aliiwezesha timu ya ZESCO kutinga nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani AFrika.
Akiwa na ZESCO, Lwandamina huyu huyu aliweza kuvitoa vigogo vya soka kama ASEC Mimosa, Wydad Casablanca na Al Ahly na kuiwezesha timu yake kutinga nusu fainali ya ligi ya mabingwa.
Yanga haikukurupuka kumchukua Lwandamina ambaye pia haikuwa kazi rahisi kum'ngoa pale ZESCO.
Bado lengo kuu la Yanga msimu huu ni kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa baada ya msimu uliopita kuboronga.
Hata hivyo kufanya vibaya kwa Yanga kwenye michuano ya Kimataifa msimu uliopita haiwezi kuwa lawama kwa Lwandamina ambaye ndio kwanza alikuwa ameichukua Yanga iliyokuwa na hali mbaya.
Ikumbukwe muda mfupi tu baada ya kuwasili Lwandamina, majanga yalianza kumuandama Mwenyekiti Yusuph Manji na kupelekea kujiweka pembeni kushughulikia kesi zake.
Msimu uliopita tulishuhudia migomo mfululizo ya wachezaji wakidai mishahara, majeruhi lakini bado Lwandamina alifanikiwa kutetea ubingwa wa tatu katika mazingira hayo magumu.
Bado naamini kocha huyu anahitaji muda kutengeneza kikosi imara kitakachokuwa tishio barani Afrika.
Kwa kuwa sasa Yanga ina falsafa ya kubana matumizi hasa baada ya Manji kuondoka, uwezo wa kununua 'majembe ya kazi' umeshuka, basi naamini Lwandamina akipewa muda wa kutosha anaweza akawatengeneza hawa waliopo na wakaweza kuisaidia timu baadae.

ADVERTISE HERE