Kulingana na taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) mapema leo, dirisha la usajili wa CAF litafungwa Julai 10 2019 ambapo baada ya hapo timu zitapigwa faini kuandikisha wachezaji wapya

Yanga ilianza zoezi la kuwaandikisha wachezaji wake mapema wiki hii kupitia mfumo wa kimtandao unaofahamika kama Cms Caf
Baada ya zoezi hilo kukamilika, bila shaka kikosi kamili cha Yanga kilichotumwa CAF kitawekwa hadharani
Nyota wa kigeni tisa ni miongoni mwa wachezaji ambao watakuwa wamesajiliwa kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao
Yanga ilifanikiwa kumalizana na nyota wake wa kigeni kwa wakati hivyo kuwa na uhakika wa kuwatumia kwenye michuano hiyo inayoanza mwanzoni mwa mwezi wa nane

ADVERTISE HERE