Balinya atua na mzuka kibao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Jul 2019
Balinya atua na mzuka kibao

Mshambuliaji mpya wa Yanga, Juma Balinya, kwa mikwara, hajambo hasa baada ya kusema anawasili nchini na vifaa vyake vyote muhimu vya kufanyia mazoezi kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Juma aliyesajiliwa na Yanga akitokea Klabu ya Polisi ya Uganda, alisema hahitaji kusubiri vifaa ya mazoezi kutoka kwa benchi la ufundi la timu hiyo, chini ya Kocha Mwinyi Zahera, kwani amejinunulia vya kwake.

Mshambuliaji huyo, aliyetarajiwa kuwasili nchini jana, alisema amepanga kuja na vifaa vya aina mbalimbali  vya kufanyia mazoezi binafsi, wakati atakapokuwa nje ya program ya kocha wake.

Mganda huyo, alisema wachezaji wengi wanashindwa kuonyesha kiwango kutokana na kutegemea kila kitu kutoka kwa benchi la ufundi au uongozi wa klabu yao.

“Nimejiwekea mfumo wa kuwa na vifaa vyangu vya mazoezi na huwa navitumia kama niko mapumziko  ili kuendelea kujiweka fiti,” Balinya amenukuliwa na gazeti la Bingwa

Alisema mipango yake kwa  sasa ni kuhakikisha anaisadia timu hiyo katika harakati ya kutwaa ubingwa wa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’