Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe yuko mbioni kukamilisha usajili kunako klabu ya Fanja Fc ya Oman
Tambwe aliondoka nchini mwezi uliopita baada ya mkataba wake kumalizika
Hata hivyo ni miongoni mwa wachezaji ambao uongozi wa Yanga uliwaruhusu waondoke kwa kuwa hawakuwa kwenye mipango ya kocha Mwinyi Zahera
Tambwe mwenye rekodi ya kufunga mabao 73 ligi kuu ya Tanzania Bara, amesema anakwenda Arabuni kupata changamoto mpya baada ya kucheza Tanzania kwa miaka sita
ADVERTISE HERE