Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema walikamilisha usajili wa Farouk Shikalo na kwamba sintofahamu iliyojitokeza itamalizwa
Zahera anayerejea Ufaransa baada ya DR Congo kuondoshwa michuano ya Afcon, amesema wakati wakimsajili mlinda lango huyo, walipewa taarifa kuwa mkataba wake ulikuwa umemalizika
Hata hivyo Bandari Fc imedai mkataba wake utamalizika Disemba
Katika hatua nyingine, Zahera amesema atarejea nchini kuendelea na majukumu ya kuinoa Yanga baada ya siku 10
Amesema wachezaji wote walioshiriki Afcon wamepewa mapumziko ya siku 10
ADVERTISE HERE