Kocha wa Ndanda ameshusha mkwara mzito

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Sep 2017
Kocha wa Ndanda ameshusha mkwara mzito
Ndanda FC tayari iko jijini Dar es salaam ambapo kesho Jumamosi itashuka kwenye dimba la Uhuru kuumana na Yanga, mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom kwa misimu mitatu mfululizo.

Musa Mbaya 'Moloto' ambaye ni kocha msaidizi wa timu hiyo kutoka kwa wala 'samaki nchanga' amesema kikosi chake hakihofii jina wala ukubwa wa Yanga na kesho wana uhakika wa kutoka na alama zote tatu.

Hata hivyo Moloto amekiri kwamba mara nyingi kikosi chake huwa na wakati mgumu kinapomenyana na Yanga jijini Dar es salaam lakini safari hii wamedhamiria kufuta uteja kwenye dimba la Uhuru.

Kabla ya kutua jijini Dar es salaam kikosi cha Ndanda kiliweka kambi mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo huo.

Mchezo wa Yanga dhidi ya Ndanda unatarajiwa kuwa na ushindani lakini wenyeji Yanga wana nafasi kubwa zaidi ya kuibuka na ushindi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’