Huyo Bui 'shughuli' yake sio ndogo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jul 2019
Huyo Bui 'shughuli' yake sio ndogo

Msimu huu Yanga imefanya usajili makini sana, kocha Mwinyi Zahera pamoja na uongozi wa timu hiyo wanastahili pongezi kwa kusajili wachezaji kulingana na mahitaji ya timu

Ukiangalia nyota wote waliosajiliwa na Yanga wametua kumaliza changamoto katika nafasi flani ambazo zilikuwa na madhaifu

Moja ya nafasi iliyoisumbua Yanga msimu uliopita, ilikuwa nafasi ya kiungo mkabaji

Msimu uliopita Yanga ilimtumia zaidi Fei Toto kwenye nafasi hiyo lakini sasa imemleta mtu sahihi Abdulaziz Makame 'Bui'

Bui hana mambo mengi anapokuwa uwanjani, anayajua vyema majukumu ya kiungo mkabaji

Ubora wake uko hasa kwenye kuanzisha mashambulizi.

Bui kutoka visiwani Zanzibar ana uwezo mkubwa wa kusambaza mipira kwa ufanisi

Anaweza kupiga pasi fupi na ndefu. Kwa mipira mirefu anayopiga unaweza kudhani ana rula mguuni

cut

Jambo moja la uhakika msimu huu, Yanga itakuwa bora sana kutokana na aina ya wachezaji waliosajiliwa

Kipimo chao kikubwa cha kwanza ni dhidi ya AS Vita, uwanja wa Taifa August 04 kwenye kilele cha siku ya Mwananchi

Yanga itashiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu ambapo kati ya August 09-11 itashuka dimbani kucheza mechi ya kwanza ya hatua ya awali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’