Mlinda lango mpya wa Yanga Farouk Shikalo amewaaga viongozi na wachezaji wenzake wa Bandari Fc baada ya kukamilisha majukumu ya kuitumikia timu hiyo
Shikalo amekamilisha usajili wake Yanga na atajiunga timu hiyo mkoani Morogoro baada ya kumaliza majukumu ya mwisho ya michuano ya kombe la Kagame na kikosi cha Bandari Fc
"Nilikuwa nanyi kwa misimu miwili kwa mafanikio na nimejifunza mengi nikiwa Bandari Fc," amesema
"Nipende kuwashukuru viongozi, wachezaji wenzangu na benchi la ufundi kwa sapoti yenu kubwa kwangu"
"Nawatakia mafanikio mema"
ADVERTISE HERE