Wachezaji waliokuwa na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wameanza kuripoti kambini kuungana na wenzao ambao walianza maandalizi ya msimu mpya wiki iliyopita
Mlinda lango Metacha Mnata na beki Ally Mtoni 'Sonso' wametua mkoani Morogoro kuungana na wenzao
Wachezaji waliokuwa na majukumu ya timu ya Taifa walipewa mapumziko ya siku 10
Nyota wengine akiwemo mshambuliaji Sadney Urikhob wanatarajiwa kuwasili leo
Yanga inajifua mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo dhidi ya AS Vita Club utakaopigwa August 04 siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi
Mcheoz huo pia utatumika kutambulisha kikosi kipya cha Yanga
ADVERTISE HERE