Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinatarajiwa kuingia kambini Julai 21 kujiandaa na mchezo dhidi Kenya, Harambee Stars utakaopigwa Julai 28 kwenye uwanja wa Taifa
Jana Kocha Mkuu wa timu hiyo Etienne Ndayiragije alitangaza majina ya wachezaji 26 wanaounda kikosi hicho
Yanga ambayo iko kambini mkoani Morogoro ikiendelea na maandalizi ya msimu mpya, italazimika kuwakosa wachezaji wake watano hadi baada ya mchezo huo
Wachezaji wa Yanga walioitwa kwenye kikosi cha Stars ni Metacha Mnata, Paulo Godfrey, Kelvin Yondani, Abdulaziz Makame na Feisal Salum 'Fei Toto'
ADVERTISE HERE