Mabingwa watetezi ligi kuu ya Vodacom, Yanga wameondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa kwenye dimba la Uhuru.
Bao pekee la Yanga lilifungwa na Ibrahim Ajib kwenye dakika ya 35 akiunganisha vyema krosi ya Kelvin Yondani.
Licha ya kutokuwa kwenye kiwango bora, Yanga leo ilitengeneza nafasi kadhaa za kufunga. Donald Ngoma alikosa mabao mawili huku shuti la Kamusoko likiokolewa na mlinda lango wa Ndanda.

Bado Yanga haijakuwa kwenye kiwango cha ushindani, benchi la Ufundi lina kazi ya kuirudisha timu kwenye ubora wake.
Kwani kwenye mchezo huu Yanga ingeweza kufunga mabao mengi.
Obrey Chirwa, Donald Ngoma bado hawajarejea katika viwango vyao tunavyovifahamu. Kocha George Lwandamina angejaribu kuwapumzisha kwenye baadhi ya michezo kuwapa nafasi vijana ambao wako fiti.
Lakini mwisho wa siku Yanga ilihitaji alama tatu na jambo muhimu zaidi imefanikiwa kuzipata mapungufu yaliyojitokeza naamini benchi la Ufundi litafanyia kazi.

ADVERTISE HERE