Mshambuliaji mpya wa Yanga Sadney Urikhob kutoka Namibia ametua nchini leo na kuunganisha moja kwa moja kambini mkoani Morogoro
Ujio wa Urikhob ulianza kuzungumzwa tangu juzi lakini hakuwasili hali iliyowapa hofu mashabiki wa Yanga
Hatimaye leo ametua rasmi na kuahidi kuisaidia Yanga kutwaa mataji msimu ujao
"Nimekuja kwa lengo la kuchukua makombe, tukifanya vizuri kwa ushirikiano wa timu na wachezaji wangu naamini kabisa kila kitu kinawezekana," amesema
Baada ya ujio wake, mlinda lango Farouk Shikalo ndiye pekee ambaye bado hajaripoti miongoni mwa wachezaji wa kigeni
Shikalo amepewa mapumziko ya wiki moja baada ya kumaliza majukumu ya michuano ya kombe la Kagame akiitumikia Bandari Fc
Mashabiki wanasubiri kumshuhudia Urikhob dimbani, Mnamibia huyo ana takwimu za kutisha katika kuzifumania nyavu