Licha ya jina lake kutoorodheshwa miongoni mwa wachezaji 26 ambao wataitumikia Yanga kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, mlinda lango Ramadhani Kabwili ataweza kushiriki michuano hiyo kama Mwinyi Zahera atapenda kumtumia
Dismas Ten, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga ambaye ndiye Msemaji wa timu hiyo, amesema sheria za CAF hazilazimishi mchezaji mwenye umri chini ya miaka 19 kuorodheshwa miongoni mwa wachezaji kwa ajili ya michuano hiyo
Muhimu mchezaji huyo awe amesajiliwa na timu husika, anaweza kushiriki michuano hiyo hata kama jina lake halikutumwa CAF
Kabwili ana umri wa miaka 18 hivyo amekidhi vigezo vya Sheria hiyo
Uongozi wa Yanga uliamua kumuongezea mkataba mlinda lango huyo kinda ambaye hakuna shaka baadae huenda akawa kipa wa kutegemewa wa Yanga na timu ya Taifa kutokana na umri wake kuwa mdogo
Mwaka jana Kabwili aliingia kwenye rekodi ya nyota waliocheza michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kudaka mchezo dhidi ya Township Rollers akiwa na umri wa miaka 17 tu